Sababu za utata
(a) kutumia neno lenye maana zaidi ya moja
Mfano, baba amenunua mbuzi. Neno mbuzi huweza kuwa ni mnyamaafugwae nyumbani au kifaa cha kukunia nazi. Maneno mengine yanayotoa maana zaidi ya moja ni pamoja na mkungu(mti au kifaa cha kufunikia masufuria), kombe(zawadi ya ushindi au dawa maalumu ya kunya), paa(sehemu ya juu ya nyumba au kitendo cha kuenda hewani), kupanda(kukua juu ya kitu au kuotesha mbegu ardhini)
(b) Kutozingatia taratibu za uandishi
Mfano: Tulimkuta Issa na rafiki yake Mussa
Tulimkuta Issa na rafiki yake, Mussa
Tulimkuta Issa na rafiki yake Mussa
Sentensi ya (1) ina maana kuwa tuliwakuta watu wawili yaani Juma na rafiki wa Juma aitwaye Abdi (mkato maana yake)=
Sentensi ya (2) ina maana kuwa tulimkuta juma na mtu mwingine ambaye ni rafiki wa abdi.
(c) Kutumia maneno yenye maana ya picha au maana iliyofichika mfano ‘ua’ lina maana ya
- Wigo
- kitendo cha kutoa uhai wa mtu
- Binti mzuri, hii ni lugha ya picha
(d) kutozingatia mkazo na mlegezo wa sauti. Mfano neno barabara. Linaweza kuwa na maana ya sawasawa au njia ya kupita.
(e). kutoweka wazi mtenda na mtendwa wa jambo katika sentensi. Mfano ameua samba. Inaweza kuwa samba ameuliwa au samba ameua mtu.
No comments:
Post a Comment