clock

NJIA ZITUMIKAZO KUUNDA MISIMU

NJIA ZITUMIKAZO KUUNDA MISIMU
Njia ya kufupisha maneno
Neno linaweza kufupishwa makusudi na matokeo yake kuwa ni msimu mfano kwa wanafunzi wa shule za upili katika kidato cha 5 na 6 wana vifupisho vya michepuo yao ya masomo.

Mfano: HKL (Hatusomi Kufaulu Lazima) n.k na chuo kikuu kuna neno DISCO  Mwanafunzi kutoendelea na masomo

Njia za kutohoa lugha za kigeni
Kwa kutumia utohozi tunapata misimu kama
Feg   -  kiingereza fag maana sigara
Demu  -  kiingereza Dame maana msichana


Njia ya kutumia sitiari
Sitiari ni mlinganisho wa ufanano wa umbo, rangi, kimo, dhima/kazi n.k
Baina ya vitu, misimu mingi huundwa kwa njia hii mfano......

  Njia ya kutumia tanakali
Njia hii inatumika pia katika uundaji wa misimu
Maneno kama vile
Mataputapu   -   Pombe ya kienyeji
Malapa (ndala)  -  Inatokana na sauti inayosikika wakati mtu atembeapo akiwa amevaa kandambili lap lap

(v) Njia ya kubadili maana ya msingi
Njia hii nayo imetumika katika uundaji wa misimu mfano mtu kutumia maneno kama vile kumfia, kumzimikia ina maana kumpenda sana.

No comments:

Post a Comment

<marquee>UTUMIAJI WA LUGHA</marquee>

UTUMIAJI WA LUGHA Katika utumiaji wa lugha tutaangalia ni kwa jinsi gani lugha inavyotumika katika mazingira mbalimbali ili tuu kuweza kuf...