LUGHA YA MAZUNGUMZO
Hii ni lugha inayotolewa kwa njia ya mazungumzo ya mdomo.l;ugha hii mara nyingi huwakutanisha ana kwa ana mzungumzaji na msilizaji.
SIFA ZA LUGHA YA MAZUNGUMZO
1. Ina msemaji na msikilizaji. Hii ikiwa na maana kuwa msemaji ndiye chanzo cha mazungumzo na msikilizaji ndiye kikomo.
2. Huwakutanisha ana kwa ana msemaji na msikilizaji.
3. Hubadilika badilika kutegemeana na mazingira ambayo mtu anaongea pamoja na watu. Hii huibua mitindo mbalimbali ya utumizi wa lugha.
4. Huonesha hali ya mzungumzaji mfano, hasira, chuki n.k
5. Huwasilishwa kuzungumzwa kwa sauti.
6. Mzungumzaji hutakiwa azingatie ufasaha na usanifu wa lugha, mpangilio mzuri wa mawazo, uwazi na ukweli katika maelezo yake ili aeleweke.
No comments:
Post a Comment