MAKOSA YA KISARUFI NA KIMANTIKI
Makosa katika lugha hufanywa na wazungumzaji wa lugha hiyo ama kwa kudhamiria au kwa bahati mbaya. Kwa hiyo mzungumzaji anapokiuka taratibu za lugha huweza kufanya makosa katika lugha yake, kosa hilo huweza kuwa la kisarufi ama kosa la kimantiki au maana.
Makosa ya kisarufi
Makosa ya kisarufi ni aina ya makosa ambayo hufanywa na mzungumzaji wa lugha kwa kukiuka kanuni za kisarufi za lugha hiyo.miongoni mwa makosa ambayo mzungumzaji wa lugha anaweza kuyafanya nipamoja na:
(a) Kosa la msamiati
Baadhi ya watu huchanganya msamiati wakati wa kuzungumza. Hali hii husababisha kosa la kimsamiati mfano mtu huchanganya neno mazingira na mazingara kwa kudhani maneno yote yana maana sawa, neno kuwasilisha na kuwakilisha, neno kunona na kunenepa.
(b) Kosa la kimuundo.
Makosa ya kimuundo hujitokeza kwa sababu ya kukiuka miundo ya sentensi ya Kiswahili.
Mfano: mfano sentensi za Kiswahili huanza na nomino halafu hufuata kivumishi. Lakini baadhi ya watu huanza na kivumishi ikafuata nomino.mfano, mtundu mtoto ameadhibiwa ambapo usahihi ni mtoto mtundu ameadhibiwa
(d) Kosa la kimatamshi
Makosa ya kimatamshi nayo ni sehemu ya makosa ya kisarufi watu wengine hushindwa kutamka baadhi ya maneno (sauti) ya lugha ya kishwahili sanifu.
Kura na kurara je? - Kula na kulala je?
Selasini na thaba - Thelathini na saba
Achante chana - Ahsante sana
Nke wako - mke wako
(e) kosa la kuacha vitamkwa.
Hili ni kosa la kisarufi ambalo mzungumzaji hudondosha baadhi ya vitamkwa au maneno katika sentensi hali ambayo hupeleka kutoa taarifa tofauti. Mfano. Baba ameondoka kazini badala ya baba ameondoka kwenda kazini.
(f) kosa la kuongeza maneno au vitamkwa.
Baadhi ya wazungumzaji hujaribu kuongeza vitamkwa visivyo na umuhimu katika sentensi. Mfano naondokaga, nampendaga, sijakwambiaga, simpendagi.
shwari kabisa
ReplyDeletevery useful
ReplyDeleteMatini safi kabisa
ReplyDelete