AINA ZA REJESTA
Rejesta za mitaani
Haya ni mazungumzo yanayozungumzwa magengeni au katika makundi ya vijana wa rika moja nayo hueleweka na wazungumzaji wenyewe wenye utamaduni mmoja.
Mfano. John: Oya mshkaji wangu dingo anasumbua ile kinoma.
Faridi: amekwama wapi kwani?
Rejesta ya hotelini.
Huu ni mtindo unaotumika hotelini, hutumia lugha ya mkato ili kutopoteza muda na kuyafanya mazungumzo yawe mafupi.
Mfano: muuzaji: nani wali maharage.
mteja: hapa.
Rejesta za hospitalini.
Ni mtindo wa lugha unaotumiwa na wahudumu, madaktari, wauguzi na wagonjwa hospitalini. Lugha hii huwa ya upole, mkato ili kumjenga mgonjwa na ndugu wa karibu matumaini.
Mfano, daktari: kunywa mbili Mara tatu ( yaani asubuhi vidonge viwili, mchana viwili na usiku viwili)
Rejesta ya kanisani.
Lugha hii hutumika kanisani ambayo hutofautiana na mazingira mingine kutokana na uteuzi na mfuatano wa maneno yanaendana na shughuli ya kanisani tuu ambayo ni maneno ya ibada. Mfano bwana yesu asifiwe, haleluya n.k
Rejesta ya mahakamani.
Hizi ni rejesta ambazo hutawaliwa na mazungumzo rasmi katika shughuli mbalimbali za kimahakama. Katika uzungumzaji huwepo mfuatano wa maelezo na hoja zenye ukweli uliofanyiwa upelelezi na hakuna lugha ya kukatisha.
Mfano:
Mheshiwa hakimu nimekubaliana na maelezo ya shahidi.
Baadhi ya misamiati ya mahakamani ni pamoja na mshitakiwa, hakimu, kesi, mlalamikaji, kifungo.
Nan alieandika nakala hii nataka reference
ReplyDelete