MAMBO YANAYOSABABISHA KUTOKEA KWA REJESTA
Ubinafsi/ upekee
Ni utofauti kati ya watumiaji wa lugha ambapo mtu huweka tufauti zitakazo mtafautisha na mtu mwingine, Yaani tabia aliyonayo mtu ya muda wa kudumu kila mtu ana namna ya kuzungumza ambapo humtofautisha na watu wengine hali hii huleta ubinafsi katika sauti yake (matamshi) na mwisho huleta mtindo wa pekee ambao ni tofauti na wengine.
Mwingiliano
Makundi ya watu mbalimbali yanapochangamana husababisha mwingiliano miongoni mwao na ili kuweza kutofautisha kundi moja na kundi jingine kuna mambo fulani ambayo hutofautiana miongoni mwa makundi hayo na mambo hayo katika lugha huhusisha matamshi ya maneno, mpangilio wa maneno (sarufi) tofauti hizi husababisha mitindo miwili tofauti miongoni mwa makundi hayo hivyo husababisha kuzuka kwa rejesta.
Kupita kwa wakati
Kila kipindi na mitindo yake katika kila mahali. Na hii ni kutokana na mabadiliko ya kihistoria yanayoikumba jamii fulani kila kipindi cha mpito wa kihistoria huweza kuwa na maneno yake ambayo huwa ni tofauti na kipindi kingine cha kihistoria. Vilevile mitindo ya lugha kutoka kipindi kimoja hadi kingine huweza kuwa tofauti. Hivyo rejesta huweza kutoka kati ya kipindi kimoja na kingine.
Mfano: enzi za ukoloni, uhuru, azimio la Arusha, hali ngumu ya maisha n.k
Shughuli iliyopo
Hapo hutegemeana na mazingira gani ambayo shughuli hiyo inafanyika mfano; msikitini, kanisani, darasani, mahakamani, hotelini, hospitalini, shughuli fulani katika mazingira fulani hutupatia rejesta za mahali.
Tofauti za hadhi za wahusika (Uhusiano wa wahusika)
Mfano; wasomi au wasiosoma, mwajiri/ mwajiriwa, tajiri/ maskini, hali hii kwa ufupi husababishwa na matabaka yaliyopo katika jamii. Tabaka moja na tabaka jingine hutumia lugha ambayo huwa ni tofauti miongoni mwao hivyo husababisha rejesta kuzuka miongoni mwa matabaka hayo.
Matumizi ya uficho tafsida
Hali hii pia husababisha kuzuka kwa rejesta kwani husababisha mitindo mbalimbali miongoni mwa wazungumzaji mfano: mwanaume mwenye mambo ya kike huitwa shoga, punga, bwabwa n.k.
Shukran kazi nzuri
ReplyDelete